Luke 7:1-6

Isa Amponya Mtumishi Wa Jemadari

(Mathayo 8:5-13)

1 aBaada ya Isa kumaliza kusema haya yote watu wakiwa wanamsikiliza, akaingia Kapernaumu. 2 bMtumishi wa jemadari mmoja wa Kirumi, ambaye bwana wake alimthamini sana, alikuwa mgonjwa sana karibu kufa. 3Jemadari huyo aliposikia habari za Isa, aliwatuma wazee wa Kiyahudi kwake, wakamwomba aje kumponya mtumishi wa huyo jemadari. 4Wale wazee walipofika kwa Isa, wakamsihi sana amsaidie yule jemadari wakisema, “Mtu huyu anastahili wewe umfanyie jambo hili, 5kwa sababu analipenda taifa letu tena ametujengea sinagogi.” 6Hivyo Isa akaongozana nao, lakini alipokuwa hayuko mbali na nyumbani, yule jemadari akatuma rafiki zake kumwambia Isa, “Bwana, usijisumbue, kwani mimi sistahili wewe kuingia chini ya dari yangu.
Copyright information for SwhKC